Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akiwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mihama utakaojengwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) leo Jumanne Mei 10, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akiwasili katika eneo lililotengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mihama utakaojengwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) leo Jumanne Mei 10, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akiwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mihama utakaojengwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) leo Jumanne Mei 10, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mihama katika eneo lililotengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mihama utakaojengwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) leo Jumanne Mei 10, 2022.

*******************
Na Samir Salum, Lango la Habari-MWANZA
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla ametembelea eneo la ujenzi wa zahanati ya Mihama katika Kata ya Kitangili unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Masalla ametembelea eneo hilo leo Jumanne Mei 10, 2022 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika Kata Zilizopo wilayani ilemela Mkoani Mwanza ikiwa na kauli mbiu ya “Ongea na DC Mtaani Kwako”.
Akizungumzia kuhusu mradi huo Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Frank Ngitaoh, amesema kuwa ujenzi wa zahanati ya Mihama utagharimu shilingi milioni 180 ambapo Asilimia 90 zitatolewa na TASAF huku asilimia 10 zitachangiwa na wananchi.
“fedha hizi zitajenga zahanati kwa hatua zote pamoja na vifaa vya ndani pamoja na wodi ya kujifungulia, pia tutajenga nyumba moja ya Mganga” amesema Frank
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla amesema kuwa ujio wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kutekeleza mradi huo ni kutokana na jitihada za Uongozi wa Wilaya na Kata hiyo kutokana na wananchi kulalamikia kero ya ukosefu wa huduma ya afya katika Kata ya Kitangili.
Aidha amewapongeza Wananchi wa Mtaa wa Mihama kwa jitihada zao katika ujenzi wa mradi huo wa zahanati kuchimba msingi, kuchangia kokoto, mawe pamoja na kutoa michango mbalimbali ya kifedha huku akielekeza uongozi wa kata kusimamia michango ya wananchi ili kufikia asilimia 10 zinazohitajika.
“Jitihada za uwepo wa zahanati katika mtaa huu zimeanzishwa na uongozi wa Wilaya na Kata kutokana na malalamiko yenu wananchi, pia niwapongeze ninyi kwa kujitolea katika ujenzi wa zahanati hii” amesema DC Masalla
Naye Diwani wa Kata ya Kitangili amesema ujenzi wa zahanati hiyo utasaidia kupunguza kero ya ukosefu wa huduma ya afya kwa wananchi na kupongeza juhudi za Serikali ya awamu ya sita kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kufadhili mradi huo.
Mwisho