Breaking

Monday, 23 May 2022

NAIBU WAZIRI WA MADINI ZIMBABWE ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU MWANZA

Naibu Waziri wa Madini na Uendelezaji Migodi wa Zimbabwe, Dkt. Polite Kambamura (katikati) akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Madini nchini Dkt. Steven Kiruswa alipotembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza (Mwanza Precious Metals Refinery) kilichopo Wilayani ilemela Jijini Mwanza leo Jumatatu Mei 23, 2022.

Naibu Waziri wa Madini na Uendelezaji Migodi wa Zimbabwe, Dkt. Polite Kambamura (katikati) akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Madini nchini Dkt. Steven Kiruswa wakisikiliza maelezo alipotembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza (Mwanza Precious Metals Refinery) kilichopo Wilayani ilemela Jijini Mwanza leo Jumatatu Mei 23, 2022.

Naibu Waziri wa Madini na Uendelezaji Migodi wa Zimbabwe, Dkt. Polite Kambamura (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Madini nchini Dkt. Steven Kiruswa( katikati) alipowasili katika kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza (Mwanza Precious Metals Refinery) kilichopo Wilayani ilemela Jijini Mwanza leo Jumatatu Mei 23, 2022.

Naibu Waziri wa Madini nchini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza katika kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza (Mwanza Precious Metals Refinery) kilichopo Wilayani ilemela Jijini Mwanza leo Jumatatu Mei 23, 2022.

Naibu Waziri wa Madini na Uendelezaji Migodi wa Zimbabwe, Dkt. Polite Kambamura (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Madini nchini Dkt. Steven Kiruswa( katikati) alipowasili katika kiwanda cha kusafisha dhahabu Mwanza (Mwanza Precious Metals Refinery) kilichopo Wilayani ilemela Jijini Mwanza leo Jumatatu Mei 23, 2022.

*********

Na Samir Salum, Lango la habari

Naibu Waziri wa Madini na Uendelezaji Migodi wa Zimbabwe Dkt. Polite Kambamura ameanza ziara ya kikazi ya siku tano nchini kwa lengo la kujifunza uendeshaji na usimamizi wa sekta ya madini.

Dkt. Kambamura ameanza rasmi ziara hiyo leo Jumatatu Mei 23, 2022 ambapo akiongozwa na mwenyeji wake ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Nchini Dkt. Steven Kiruswa ametembelea Kiwanda cha kusafisha dhahabu (Mwanza Precious Metals Refinery) kilichopo Wilayani ilemela Jijini Mwanza .

Akiwa kiwandani hapo, Dkt. Kambamura amevutiwa na kiwanda hicho ambacho kinamilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na mwekezaji binafsi chenye uwezo wa kusafisha kilo 480 za dhahabu kwa siku kwa ubora wa asilimia 99.9.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini Tanzania, Dkt.Kiruswa amesema, ushirikiano wa Tanzania na Zimbabwe kwenye Sekta ya Madini ni wa kujengeana uwezo kwa kuwa Zimbabwe imepiga hatua kubwa kwenye sekta ya madini kupitia wawekezaji wakubwa.

Naye, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Deusdedith Magala akizungumza kwa niaba ya STAMICO amesema kiwanda hicho cha kusafisha dhahabu cha Mwanza kitafanya wafanyabiashara wa Zimbabwe wavutiwe kupeleka dhahabu yao kwa ajili ya kusafishwa kutokana na kuwepo kwa mazingira wenzeshi ya uwekezaji hapa nchini.

Naibu Waziri wa Madini Zimbabwe na ujumbe wake watakuwa nchini kwa ziara ya siku tano ambapo Katika ziara hiyo watatembelea mgodi wa dhahabu wa GGM, wachimbaji wadogo wa Nyarugusu na wachimbaji wadogo wa almasi wa Shinyanga.

Mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages