Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeipiga faini ya USD 10,000– (Takriban Tsh. Milioni 23) Klabu hiyo baada ya kupatikana na hatia kuwasha moto katika uwanja wa Orlando katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates.
Kabla ya mchezo huo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho, Wachezaji wa Simba walionekana kukusanyika katikati ya uwanja na baadaye moshi kutokea katikati ya kundi hilo.
Taarifa kutoka CAF imesema Maafisa wa mchezo walionesha katika ripoti zao kwamba “Wachezaji wa Simba waliwasha moto katikati ya uwanja wakati wakijifanya kuomba kabla ya mechi. Ilitubidi kumwaga maji ili kuuzima moto”
CAF imeongeza kuwa malipo hayo yanapaswa kufanyika ndani ya siku 60.