Breaking

Sunday, 15 May 2022

SHAKA ATAKA UAMUZI WA KUWAPANGA WAMACHINGA USIWAPE UMASIKINI WANANCHI

 




KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema uamuzi wa serikali kuwapanga vyema wafanyabiashara wadogo hauna lengo la kuwatia umasikini bali kuwajengea mazingira mazuri ya kujiongezea kipato.

Shaka aliyasema hayo Jumamosi Mei 14, 2022 mjini Babati wakati akizungumza na wajasiriamali wadogo wanaofanya shughuli zao katika stendi ya zamani mjini Babati, mkoa wa Manyara ambao walilalamikia uamuzi wa kuwahamisha katika eneo hilo huku wakisema walikopelekwa kuna mazingira magumu ya biashara.



Wafanyabiashara hao wakiwemo wakinamama wamelalamikia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo ikiwemo ya kusumbuliwa na mgambo wa Halmashauri.

Kutokana na malalamiko hayo Shaka amesema ni vyema viongozi hususan wa Halmashauri za wilaya kuhakikisha hawapindishi lengo hilo kwa kuwawekea wamachinga mazingira magumu ya kufanyia biashara.

"Uamuzi wa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwapanga wamachinga katika maeneo rasmi hauna maana ya kuwatengenezea umasikini, bali kuwawekea mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuongezea kipato," alisema.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages