Na Said Muhibu, Lango La Habari
Watu saba wamefariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa katika ajali ya moto kwenye meli nchini Ufilipino hii leo jumatatu ya Mei 23, 2022.
Ripoti iliyotolewa na shirika la habari la Aljazeera imeeleza Meli hiyo iliyobeba watu 134 ilishika moto siku ya Jumatatu kabla ya kufika bandari ya Real katika jimbo la Quezon, takriban kilomita 60 (maili 37.28) mashariki mwa mji mkuu wa Manila. Ilikuwa imeondoka kwenye Kisiwa cha Polilio saa kumi na moja asubuhi kwa saa za huko na kuua watu saba huku watu 23 wakijeruhiwa na wengine 120 kuokolewa.
Chanzo cha moto huo hakijabainika bado, lakini Ufilipino, nchi ya visiwa zaidi ya 7,600, ina rekodi mbaya ya usalama wa baharini,na matukio mfano wa hayo huripotiwa mara nyingi.