Breaking

Tuesday, 31 May 2022

RAIS SAMIA APOKEA KOMBE LA DUNIA, AWATAKA WATANZANIA KULISHUHUDIA KWA MKAPA KESHO

Na John Mapepele


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan leo Mei 31, 2022 amepokea kombe la Dunia la FIFA Ikulu jijini Dar es Salaam  ambalo litakaa kwa siku mbili kabla ya kuondoka kesho kutwa.


Kombe hilo amekabidhiwa na mchezaji mkongwe duniani wa Brazil Juliano Belletti ambaye anaongoza timu ya ziara ya kombe hilo nchini.

Tanzania inakua miongoni mwa nchi tisa za Afrika  ambazo imepata bahati ya kupitiwa na kombe hilo.


Akipokea kombe hilo Rais Samia amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Juni 1, 2022 kufika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kupiga  picha na kombe hilo.

Amesema kuwa Tanzania imechaguliwa kuwa miongoni mwa nchi hizo kutokana na kuendelea kufanya vizuri kwenye Michezo ambapo amesema watanzania wengi wanapenda soka.


Aidha, ametoa rai kwa watanzania kutumia ujio wa kombe la Dunia nchini kuitangaza  Tanzania duniani.

Kesho kombe litaanza kuonyeshwa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni na baada ya hapo kutaonyeshwa filamu ya Royal tour ambayo Mhe. Rais Samia ameshiriki.


Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, amemshukuru Mhe.Rais kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye Michezo katika kipindi kifupi cha utawala wake.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages