Breaking

Friday, 13 May 2022

PHILIP COUTINHO SASA MALI HALALI YA ASTON VILLA



Na Ayoub Julius,Lango la Habari 


Kiungo raia wa Brazili Philip Coutinho  amesaidi mkataba wa kudumu na Aston Villa,Mchezaji huyo wa Brazil ametia saini kandarasi hadi 2026 akitokea Barcelona. 


Baada ya kusainiwa kwa mkopo kutoka kwa wababe hao wa Catalan mnamo Januari, Coutinho aliisaidia moja kwa moja Villa kwa uchezaji bora. 


Amefunga mabao manne na kutoa pasi tatu za mabao hadi sasa. 


Kocha Mkuu Steven Gerrard alisema: “Huu ni usajili mzuri wa Aston Villa.Phil ni mtaalamu wa kuigwa na athari yake kwenye timu imekuwa wazi tangu alipojiunga mwezi Januari".  


"Kwa jinsi anavyojiendesha ndani na nje ya uwanja, yeye pia ni mfano muhimu kwa wachezaji wetu wachanga ambao wanaweza kufaidika tu kutokana na uzoefu wake". 


"Tunapotarajia kujiandaa kwa msimu ujao, ni ajabu kufanya kazi katika klabu ambayo inatekeleza shughuli zake kwa uthabiti na kwa urahisi." 


Coutinho alikipiga katika klabu ya Liverpool kwa mafanikio makubwa na kisha kutimkia nchi Hispania kujiunga na miamba wa Catalani na baadae akatimkia kunako klabu ya Buyern Munich kwa mkopo mpaka pale alipojiunga na Aston Villa kwa mkopo na sasa amesaini mkataba wa kudumu mpaka mwaka 2026.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages