Vijana wanaodhaniwa kuwa ni Panya road wamewakata mapanga watu 19 katika mtaaa wa Mtongani, Kata ya Kunduchi mkoani Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2022.
Tukio hilo limetokea masaa kadhaa tu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alipotoa onyo kwa vikundi hivyo kuachana na tabia hiyo, wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika mkoani Dodoma.
Mmoja wa majeruhi hao amesema kwamba, vijana hao walikimbilia ndoo ya pesa, huku wakimuwahi kwa kumkata mikono yake ili akose namna ya kupambana nao.
Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi
Source: EATV