Breaking

Wednesday, 25 May 2022

OFISI YA MSAJILI YAMSIMAMISHA MBATIA KUJIHUSISHA NA SIASA




Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini imebariki Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Sekretarieti yake yote kusimamishwa na kuwataka kutojihusisha na siasa ndani ya chama hicho hadi uamuzi huo utakapoamuliwa vinginevyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Mei 25, 2022 na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza akisema uamuzi wa Kikao cha Halmashauria ya chama hicho kilichofanyika Mei 21 mwaka huu, ulikuwa halali kwa akidi ya wajumbe wake licha ya kutotaja uhalali wa akidi hiyo.

“Baada ya kusimamishwa, katibu wa chama hicho alituletea barua kwa fomu ya kisheria inayotujulisha kusimamishwa uanachama, tumekubaliana na uamuzi huo. Kama hawataridhika (Kina Mbatia) ziko njia za kutafuta haki, waende mahakamani,”amesema Nyahoza.

Mei 21, 2022 Halmashauri Kuu ya Chama hicho ilimsimamisha Mbatia na Makamu Mwenyekiti Bara Angelina Mtaigwa kujihusisha na shughuli zozote za Chama hicho mpaka watakapoitwa kujieleza katika mkutano Mkuu wa Wanachama wa Chama hicho, uamuzi ambao hata hivyo Mbatia na wenzake waliupinga.

Soma zaidi : NCCR MAGEUZI YAMSIMAMISHA MBATIA NA MAKAMU WAKE

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages