Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Masanja (Mb) akiwa ameongozana na Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa (katikati) pamoja na Mawaziri wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Mazingira, Maliasili na Utalii kutoka nchi za Zambia, Namibia na Botswana, kutembelea mabanda ya washiriki ambao ni wazawa wa Zimbabwe, katika Tamasha la Utalii wa Utamaduni la kutangaza vyakula vya asili lililofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Elephant Hills Eneo la Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa tatu kushoto) akifuatulia matukio katika Tamasha la Utalii wa Utamaduni la kutangaza vyakula vya asili lililoandaliwa na Serikali ya Zimbabwe, lililofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Elephant Hills kwenye eneo la Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi katika Tamasha la Utalii wa Utamaduni la kutangaza vyakula vya asili lililoandaliwa na Serikali ya Zimbabwe, lililofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Elephant Hills kwenye eneo la Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakifuatilia matukio katika Tamasha la Utalii wa Utamaduni la kutangaza vyakula vya asili lililofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Elephant Hills Eneo la Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Masanja (Mb) (kulia) akiwa ameongozana na Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa (katikati) pamoja na Mawaziri wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Mazingira, Maliasili na Utalii kutoka nchi za Zambia, Namibia na Botswana, kutembelea mabanda ya washiriki ambao ni wazawa wa Zimbabwe, katika Tamasha la Utalii wa Utamaduni la kutangaza vyakula vya asili lililofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Elephant Hills Eneo la Victoria Falls nchini Zimbabwe.
************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania kuhudhuria katika Tamasha la Utalii wa Utamaduni la kutangaza vyakula vya asili lililoandaliwa na Serikali ya Zimbabwe, lililofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya Elephant Hills katika eneo la Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Akizungumza baada ya tamasha hilo Mhe. Masanja amesema tamasha hilo ni fursa ya kipekee ya kutangaza Utalii wa Utamaduni kupitia vyakula vya asili hivyo Tanzania inaweza kuiga mfano huo wa kutangaza vyakula vya asili ili kuvutia watalii wengi zaidi.
Mhe. Masanja ameshiriki katika kutembelea mabanda ya washiriki ambao ni wazawa wa Zimbabwe, akiwa ameongozana na Mke wa Rais wa Zimbabwe, Dkt. Amai Auxillia Mnangagwa pamoja na Mawaziri wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii, Mazingira, Maliasili na Utalii kutoka nchi za Zambia, Namibia na Botswana, na kisha kushiriki katika zoezi la kugawa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.
Mhe. Masanja yupo nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki kwenye Kongamano la Tembo wa Afrika litakalofanyika katika Hifadhi ya Taifa Hwange ikiwa na lengo la kuunda mpango mpya na bora zaidi wa uhifadhi wa Tembo na kukuza Utalii Barani Afrika.