Na Samir Salum, Lango la habari
Hayo yameelezwa Mei 15, 2022 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Kigahe amesema kuwa Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakumba wajasiliamali na wafanyabiashara wadogo ikiwemo kukosekana kwa maeneo rafiki ya kufanyia biashara zao hali inayowafanya kushindwa kukuza kipato.
Amesema Serikali iko bega kwa bega na wajasiliamali hao ili kuhakikisha wanafikia malengo yao katika kukuza kipato chao na kuongeza wigo wa uchumi nchini.
"Niwaahidi kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zote zitakazo jitokeza ili kuwaboreshea Biashara zenu na kukuza kipato" Amesema
Aidha ameongeza Kuwa Serikali Kupitia Wizara ya Viwanda na biashara inalitambua Rasmi Tamasha hilo la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa huku akiwapongeza waandaaji wa akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge na Mkurugenzi wa Kangaroo Event Shaban Mikongoti kwa kufanikisha k.
Tamasha kubwa la wajasiliamali na kuhamasisha Sensa Kanda ya ziwa limefanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kuanzia May 09, 2022 hadi May 15, 2022 likiwa na kauli mbiu ya "Jitokeze kuhesabiwa August 23, 2022 kwa maendeleo ya Taifa".
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akitembelea Mabanda ya Wajasiliamali katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa liliofanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akitembelea Mabanda ya Wajasiliamali katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa liliofanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akizungumza wakati akifunga Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa liliofanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga. Mei 15, 2022
Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe wakati akizungumza katika Kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (Kulia) katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022
Mkurugenzi wa Kangaroo Event Shaban Mikongoti Akizungumza katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge (Katikati) na Mkurugenzi wa Kangaroo Event Shaban Mikongoti (kulia) katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akimkabidhi Toffee Up Town cheti cha uhamasishaji bora wa Tamasha Katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akikabidhiwa Zawadi ya viungo vya chakula na mjasiliamali kutoka Arul products katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge na Mkurugenzi wa Kangaroo Event Shaban Mikongoti wakimkabidhi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe Picha iliyotengenezwa na wajasiliamali katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022.
Msanii Bando Mc akitoa Burudani katika kilele cha Tamasha la Wajasiliamali Kanda ya Ziwa Mei 15, 2022.