Mchezaji wa Simba, Bernard Morrison anashikiliwa katika kituo Cha Polisi Cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumjeruhi shabiki wa Yanga na kitu chenye ncha kali.
Mkuu wa Kituo Cha Polisi Chang’ombe, ASP Mohammed Simba amethibitisha kupokea kesi hiyo “Ndio tumepokea hiyo kesi na tunaendelea na mahojiano tukikamilisha tutawajulisha,”
Tukio hilo limetoka mara baada ya Derby ya Kariakoo kutamatika katika uwanja wa Benjamin Mkapa hii leo.
Source: Wasafi Media