Breaking

Thursday, 12 May 2022

MBUNGE KISHAPU AWATAKA MADIWANI, WATAALAMU KUHAMASISHA ZOEZI LA SENSA





Na Seveline Mbullu, Lango La Habari-Kishapu

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo Amewataka Madiwani na wataalamu wa idara mbali mbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kuwa mabalozi wa Wazuri wa Sensa ya watu na Makazi itakayo fanyika Tarehe 23 August 2023.

Butondo ameyasema hayo Jumatano Mei 11, 2022 katika Baraza la Madiwani lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.


Amesema kuwa zoezi la sensa litasaidia Serikali kupanga vyema shughuli za kimaendeleo na kuwataka Madiwani na Waatalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Kusimamia Zoezi hilo.

"niwaombe madiwani wenzangu na wataalamu tuhakikishe zoezi hili la Sensa tunafanikiwa Kwa Kiasi kikubwa kama tulivyo fanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye Zoezi la Positikodi na kufanikiwa kuongoza ki mkoa na Sensa tukafanye vizuri zaidi" Amesema Butondo

Aidha, Butondo alitumia furusa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Fedha nyingi Ambazo zinakwenda kutekeleza miradi mingi ambayo ipo katika Jimbo hilo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages