Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imesema Wabunge 19 waliovuliwa uanachama na CHADEMA, waendelee kufanya shughuli zao za kibunge hadi Mahakama itakaposikiliza maombi yao ya zuio la muda kuhusu ubunge wao.
Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Mei 16, 2022 na Jaji John Mgeta baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Wabunge hao waendelee kuwa Bungeni ama laah, ambapo June 13, 2022 ndio atasikiliza zuio hilo.