Breaking

Thursday, 12 May 2022

MADIWANI KISHAPU WALAANI UKIUKWAJI WA SHERIA UNAOFANYWA NA WATUMISHI WA MGODI WA AL HILAL, LAWEKA MAAZIMIO JUU YA MWEKEZAJI




Na Seveline Mbullu, Lango La Habari-Kishapu

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu limelaani vikali Vitendo vya Ukiukwaji wa Sheria unaofanywa na watumishi wa Mgodi wa Almasi wa AL HILLAL.

Hayo yamejiri Jumatano Mei 11, 2022 na kuwasilishwa kwa hoja Binafsi kutoka kwa Diwani wa kata ya Songwa Abdul Ngolomole kuhusu Muwekezaji wa Mgodi wa AL HILAL kusimama kwa muda mrefu kuzalisha Almasi pamoja na kudaiwa mapato ya Halmashauri kwa Muda mrefu.


Kutokana na hoja hizo Baraza la Madiwani liliamua kufanya maazimio kwa muwekezaji wa Mgodi huo AL HILAL.

Akisoma maazimio hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu William Jijimya ameeleza kuwa Baraza limemtaka Muwekezaji wa Mgodi huo kutoa sehemu ya eneo la ardhi anayoimiliki kwajili ya wachimbaji wadogowadogo ili kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo katika eneo hilo.


Pia mwekezaji ametakiwa kuanza mara moja kuzalisha almasi ili kuiwezesha Halmashauri kupata mapato yake Vinginevyo aachie eneo hilo.

Aidha mwekezaji huyo ametakiwa kulipa Deni la ushuru wa huduma (service levis) analodaiwa kwa muda wote na Halmashauri na kutoa Fedha kwa kwajili uwajibikaji katika jamii(CSR)




Mwisho.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages