Breaking

Saturday, 28 May 2022

YANGA WATETEMA MBELE YA SIMBA, WATINGA FAINALI ASFC



Na Ayoub Julius, Lango La Habari


Klabu ya Yanga Sc imefanikiwa kufuzu katika hatua ya Fainali ya kombe la shirikisho la Azam kwa kuwachapa mahasimu wao Simba Sc kwa Bao 1-0


Bao la Yanga Sc limewekwa kimyani na kiungo machachari Feisal Salumu 'Fei Toto' mnamo dakika ya 25' ya mchezo kipindi cha kwanza.


Yanga Sc anakwenda kucheza Fainali dhidi ya Mshindi kati ya Azam na Costal Union mchezo utakao chezwa siku ya kesho Tarehe 29 Mwezi Mei 2022 saa 9:30 Alasiri.

Aidha Yanga amemvua ubingwa Mtani wake rasmi hii leo baada ya kipigo hicho.

Simba Sc ndiye aliyekuwa mtetezi wa taji hilo la Shirikisho la Azam akishinda taji hilo msimu uliopita 2020/2021
















Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages