Breaking

Tuesday, 17 May 2022

KOCHA, MENEJA MBEYA KWANZA WAFUNGIWA MIAKA MITANO, NAMUNGO WAPEWA POINT




Kocha Mbwana Makata na Meneja David Naftali wa Mbeya Kwanza wamefungiwa kwa kipindi cha miaka mitano kila mmoja kwa kosa la kushawishi/kuamuru wachezaji wasiingie uwanjani kuanza mchezo tukio lililosababisha mchezo wa timu yao dhidi ya Namungo FC kutofanyika.

Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imeipa Namungo FC pointi 3 na mabao matatu na kusema kuwa imejiridhisha Mbeya Kwanza waligomea mchezo huo licha ya taratibu kuwa sawa dakika ya 23 ikiwa ni dakika saba kabla ya kutimu nusu saa.

Aidha, Kocha wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma na mchezaji wa timu hiyo, Jamali Mtegeta wamefungiwa michezo mitatu na faini ya Tsh 500,000 kila mmoja kwa kosa la kushambuliana kwa mateke wakati wa mechi ya timu yao dhidi ya Biashara United, Mei 5, 2022.











Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages