Breaking

Wednesday, 18 May 2022

KATAMBI ATOA MAJIBU KWA VIJANA AMBAO HAWAJAPATA MIKOPO




Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu, Vijana, Kazi na Ajira, Patrobas Katambi, amesema kwamba zaidi ya bilioni 150 zimekwishatolewa kwa vijana kama mikopo na kusema kama kuna kijana yeyote ambaye hajapata mkopo itakuwa pengine ni Mkenya.

Katambi amesema hayo leo Mei 18, 2022 bungeni mjini Dodoma, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda, aliyehoji  vijana kutopata ajira kwa zaidi ya miaka sita sasa pamoja na kwamba kuna mfumo wa utoaji wa mikopo katika halmashauri , hivyo mfumo huo unawatupa  nje.

“Ukiangalia hakuna kijana yeyote ambaye hapati mkopo, kumekuwa na scheme za utoaji mkopo katika elimu, sekondari tumekuwa tukitoa elimu bila malipo, chuo kikuu anakutana na Bodi ya Mikopo, akitoka chuo akienda kwenye halmashauri zetu tunatoa mikopo.

“Pia tumekuwa na scheme za makubaliano na mabenki mbalimbali kushusha riba na kutoa mikopo, kama mtapitisha bajeti ya Wizara ya Kilimo, kule kuna mpango wa 'Building the better tomorrow' utakaogusa zaidi ya vijana milioni 1, ili kutengenezewa scheme za kilimo,”  amesema Sophia


"Sisi kama serikali tunazotakwimu za vijana hawa, na wale wote wanaofanya application za ajira, vyuo vikuu vyote tumekuwa tukipata taarifa, tunao vijana zaidi ya laki mbili wanaoingia kwenye soko la ajira kutoka vyuo mbalimbali, pia tuna mifumo na programu tunazoziandaa ikiwa ni pamoja na internship, kuangaliziwa ajira ndani na nje ya nchi,"amesema Katambia

Aidha Katambi ameongeza kuwa, "Tumekuwa tukiendelea kutoa mikopo na zaidi ya bilioni 150 zimekwishakutolewa kwa vijana mbalimbali, kama kuna vijana ambao wapo labda pengine sio Watanzania ni Wakenya utanisaidia niweze kuwaingiza hapa tuone namna gani tunawasaidia.


Source: EATv
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages