Breaking

Wednesday, 4 May 2022

IGP SIRRO ATOA ONYO KALI KWA PANYA ROAD




Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amekitaka kikundi cha 'Panya Road' kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani na kwamba Jeshi hilo limejipanga kukabiliana na watu hao.


IGP Sirro amesema hayo leo Jumatano May 04, 2022 wakati alipofanya ziara katika Kata ya Kunduchi Mtongani na Kata ya Kawe jijini Dar es salaam na kuwapa pole watu waliojeruhiwa na kikundi hicho cha Panya Road.


"Panya road nawapa salamu kama unataka maisha yako yawe vizuri acha hiyo kama ulikuwa na panga lako nenda kalitupe mahala pengine," amesema IGP Sirro


Aidha, IGP Sirro amesema ni vyema wazazi na walezi wakaimalisha malezi ya familia zao pamoja na kushiriki kwenye vikundi vya ulinzi shirikishi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima amesema, wananchi wanahaki ya kulaumu Jeshi la Polisi ili liweze kutimiza wajibu wake wa kulinda usalama wa raia na mali zao na pia wananchi wanawajibu wa kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ili matukio ya namna hiyo yasijirudie.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages