Jeshi la kujenga taifa JKT limewaita wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kwenda kupata mafunzo ya jeshi kwa mujibu wa sheria kuanzia Juni 3 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Brigedia jenerali Mabena amesema vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka huu watatakiwa kuripotini kwenye kambi walizopangiwa kuanzia Juni 3, 2022 na kwa wale wenye ulemavu wa aina yoyote waripoti ambi ya Ruvu JKT.
"Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Kambi hii ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hii," alisema.
TAZAMA HAPA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT 2022
Jenerali Mabena ameorodhesha kambi mbalimbali ambazo watatakiwa kwenda vijana waliochaguliwa kama JKT Rwamkoma, Msange, Ruvu, Mpwapwa, Makutupora, Mafinga, Makuyuni, Kanembwa, Itaka, Mlale, Mgambo, Oljoro, Milundikwa, Nachingwea, Kibiti Bulombwa na Maramba.
Jenerali Mabena ameongeza kuwa Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa kujiunga katika mafunzo hayo ambayo yanahusisha uzalendo na stadi za kazi na maisha na utayari wa kulijenga Taifa.
TAZAMA HAPA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JKT 2022
"Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele awakaribisha vijana wote walioitwa ili kujiungna katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi na maisha, utayari kulijenga na kulitumikia Taifa," aliongezea.