Breaking

Monday, 9 May 2022

HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAITWA CHADEMA




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kwamba tayari wanachama wake 19 waliofukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho wameshapelekewa wito wa kwenda kusikiliza matokeo ya rufaa yao waliyoikata siku ya Mei 11, 2022.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 9, 2022, na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama hicho John Mrema, ambapo amesema kwamba wanachama hao wamepewa nafasi ya kufika mbele ya kikao cha Baraza Kuu na kwamba hata wasipofika haizuii majibu ya rufaa zao kutolewa.

"Tuna waliokuwa wanachama wetu 19 ambao walishafukuzwa na Kamati Kuu, walikata rufaa kwenye Baraza Kuu tunapenda kuwajulisha kwamba wameshaitwa kwa barua rasmi, wamepelekewa wito na wote wameshaupata kwa ajili ya kuja mbele ya kikao cha Baraza Kuu kusikiliza rufaa zao," amesema Mrema

Miongoni mwa wanachama waliofukuzwa na chama hicho ni Halima Mdee, Ester Bulaya, Agnesta Lambert, Esther Matiko, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba, Conchesta Rwamlaza n a wengineo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages