Breaking

Friday, 27 May 2022

HAKUNA HAJA YA CHANJO YA HOMA YA NYANI "MONKEYPOX" -WHO



Na Said Muhibu, lango la habari

Shirika la afya dunia WHO limesema hakuna haja ya kuwa na kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya nyani na badala yake watu wahimizwe kuchukua tahadhari kwa kuzuia kuenea ugonjwa huo kwa nchi ambazo bado hazijaathirika.


Kwa mujibu wa shirika la habari la Aljazeera limeeleza shirika la afya la Umoja wa Mataifa limesema mlipuko wa virusi vya homa ya nyani katika nchi zisizo na ugonjwa unaweza kuzuiwa 'kwa urahisi' ikiwa ufuatiliaji wa mawasiliano na hatua za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo zitafuatwa.


Katika mkutano wa wakala wa afya wa umoja wa mataifa uliofanyika huko Geneva leo Mei 27, 2022 urahisi," Sylvie Briand, mkurugenzi maandalizi ya magonjwa ya hatari ya kuambukiza duniani Silvie Briand alisema anafikiri juu ya kuweka hatua stahiki za kujikinga dhidi ya homa ya nyani badala ya kuweka kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo.


 "Tunafikiri ikiwa tutaweka hatua zinazofaa sasa tunaweza kuidhibiti kwa urahisi," alisema.


Ugonjwa wa homa ya nyani kwa kawaida ni maambukizi ya virusi hafifu na hupatikana katika nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Cameroon, Ivory Coast, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan Kusini na Nigeria, ikiwa ni pamoja na nchi za Magharibi mwa ulaya.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages