Breaking

Sunday, 15 May 2022

FINLAND YATANGAZA RASMI KUJIUNGA NA NATO






Na Said Muhibu, Lango La Habari 


Nchi ya Finland imetangaza kujiunga na mataifa ya wanachama wa jumuiya ya kujihami (NATO) kufuatia mzozo unaondelea kati ya Urusi na Ukraine licha ya kupewa onyo hivi karibuni na Rais wa Urusi Vladimir Putin ya kwamba kufanya hivyo ni 'kosa'.


Rais wa Finland Saul Niinisto amethibitisha hilo hii leo akiwa katika mji mkuu wa Finland Helsinki na kusema kuwa, amefanya mawasiliano ya simu na Rais Putin siku ya jumamosi na kumuelezea juu ya uamuzi huo.


Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Finland Sanna Marin alisema, anaimani wabunge wa nchi hiyo watajadili suala hilo na kuweza kuidhinisha muafaka wa uamuzi huo.


Wakati huo huo nchi ya Sweden inaweza kutangaza nia yake ya kujiunga na NATO katika siku za usoni.


Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Nato, watakaokutana mjini Berlin hii leo, wameahidi kutoa hakikisho la usalama kwa nchi za Finland na Sweden huku nia zao za kujiunga na NATO zikiidhinishwa na mataifa yote wanachama, mchakato ambao unaweza kuchukua hadi mwaka mmoja.


Putin hajatoa tishio mahususi kuhusu hatua hiyo ya Finland, lakini wizara ya mambo ya nje ya Urusi imedokeza kuwa kutakuwa na kulipiza kisasi katika uamuzi huo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages