Na Said Muhibu
Tajiri mkubwa zaidi duniani Elon Musk ametangaza kuirejesha akaunti ya Twitter aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump iwapo dili lake la kupata kampuni hiyo litakamilika.
Kauli hiyo ameitoa Jumanne Mei 10, 2022 katika mkutano wa Financial Times' Future of the car, na kusema kuwa uamuzi wa Twitter kuifungia akaunti ya Trump ulikuwa ni kosa.
"Nadhani haikuwa sahihi kuipiga marufuku akaunti ya Donald Trump, nadhani lilikuwa ni kosa," Musk alisema.
Akaunti ya Twitter ya Donald Trump ilizuiwa mnamo mwaka 2021 kufuatia mandamano ya januari 6 kwa kukiuka sheria za jukwaa dhidi ya uchochezi wa ghasia.
Hata hivyo Trump kwa upande wake amesema hatarejea kwenye Twitter hata kama akaunti yake itarejeshwa, badala yake ataendeleza ubia wake kwenye mitandao ya kijamii, Truth social ambao kufikia sasa unatatizika kujiondoa.