Breaking

Wednesday, 11 May 2022

DC MASALLA AWAASA WANANCHI ILEMELA KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Nyasaka Mkoani Mwanza leo Jumtano Mei 11, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Nyasaka Mkoani Mwanza leo Jumtano Mei 11, 2022.


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nyasaka wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Nyasaka Mkoani Mwanza leo Jumtano Mei 11, 2022.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nyasaka wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Nyasaka Mkoani Mwanza leo Jumtano Mei 11, 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla akisikiliza kero za wafanyabiashara waliopo katika soko la Nyasaka leo Jumtano Mei 11, 2022.

**************

Na Samir Salum, Lango la Habari, Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masalla ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022.

Dc Masalla ametoa rai hiyo leo Jumatano Mei 11, 2022 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Katika Kata ya Nyasaka ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika Kata Zilizopo wilayani ilemela Mkoani Mwanza ikiwa na kauli mbiu ya “Ongea na DC Mtaani Kwako”.

Amesema kuwa kutokana na ongezeko kubwa la watanzania serikali inapaswa kujua idadi ya wananchi wake ili kuiwezesha kupanga mikakati ya Utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.

sasa hivi kuna ongezeko kubwa la watu hivyo takwimu tulizonazo ni lazima tuzihuishe tujue idadiya watanzania tuliopo kwa sasa ili Serikali iweze kupanga mikakati ya maendeleo katika kila sekta” amesema DC Masalla



Aidha Dc Masalla amewashukuru wananchi wa kushiriki vyema katika zoezi la Anwani za Makazi linaloendelea Nchi nzima huku akiwaasa kuweka namba walizopewa na waratibu wa Zoezi hilo katika nyumba zao.

Amesema kuwa kuna maeneo wanachangisha fedha kwa ajili ya kuweka namba hizo ambapo ameelekeza kuwa sio lazima kuchangia kwani mwananchi anaweza kuweka anwani katika makazi yake kwa kufuata utaratibu aliopewa na waratibu wa zoezi hilo.

“zoezi la kuandika namba ni lenu wananchi, unaweza kununua rangi na kuandika namba hizo kwenye nyumba yako, rangi inayotakiwa ni njano na nyeusi, ikitokea kama Mtaa umejipanga kuchangisha basi gharama hizo zisiwaumize wananchi” amesisitiza DC Masalla


Dc Masalla ameongeza kuwa Zoezi la kuweka namba za Anuani za makazi lina faida nyingi ikiwemo kurahisisha huduma mbalimbali za kijamii na kiusalama.

MWISHO

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages