Mkuu wa wilaya ya kishapu Mhe, Joseph Modest Mkude Leo ameungana na waisilamu wa Wilaya ya Kishapu katika kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri kwenye Viwanja Vya Shirecu.
Katika Sherehe hiyo Mkude amezungumza na mamia ya waislamu waliojitokeza kwenye sala ya Eid na kuwataka wana Kishapu kudumisha umoja Amani na mshikamano uliopo kwenye Wilaya hiyo.
Aidha Mhe, Mkude ametumia furusa hiyo kuwataka wananchi Wa Wilaya hiyo kushiriki na kutoa Ushirikiano kikamilifu katika Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika tar 23 .08.2023.
"Ndugu zangu waislamu mliojitokeza Siku ya leo Naomba mkawe mabalozi wa kuhamasisha wananchi kuhusu zoezi Hili la Sensa ya watu na makazi litakalo fanyika Tar 23.08.2022 linaumuhimu mkubwa sana kwa maendeleo yetu ya Taifa kwani Bila Sensa hatuwezi kuwa na Takwimu sahihi ambazo zitaiwezesha Serikali kupanga maendeleo ya wananchi wake"
Pia Mhe, Mkude ameelezea mafanikio ya mwaka mmoja ya Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan katika Idara ya Elimu na Afya kwa kutekeleza Ujenzi wa madarasa na Vituo vya Afya katika Wilaya hiyo.