Na Ayoub Julius, Lango La Habari
Licha ya mfululizo wa matokeo mabovu katika timu ya Manchester United lakini mkongwe huyo ameendelea kung'ara kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
Ni mara ya pili katika msimu huu kwa Cristiano kutwaa tuzo hiyo ambapo tuzo yake ya mchezaji bora wa mwezi kwa msimu huu ilikuwa ni mwezi September mwaka jana (2021)
Tuzo hiyo ni zao la goli lake la 100 katika ligi kuu uingereza dhidi ya Arsenal mchezo ambao Mashetani wenkundu hao walipoteza kwa bao 3-1 bao pekee la Manchester united likifungwa na nguli huyo.
Pia katika Mchezo dhidi ya Norwich ambapo Gwiji huyo alifunga hattrick yake ya 50 ambapo Manchester United waliibuka na ushindi wa goli 3-2 na kuhitimishwa na mchezo dhidi ya chelsea uliotamatika kwa sare ya 1-1 bao pekee la Manchester United likifungwa na Cr7.
Kwa ujumla hiyo ni tuzo ya sita ya Ronaldo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa EA SPORTS, na kumfanya afikishe moja ya rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Harry Kane pamoja na Sergio Aguero.