Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kurasimisha biashara zao ili kukuza wigo wa shughuli wanazozifanya.
Wito huo umetolewa leo Alhamisi Mei 12, 2022 na Afisa Usajili wa BRELA kutoka Kanda ya Kati, Gabriel Girangay wakati wa Mkutano wa Wakandarasi unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Girangay amesema kuwa urasimishaji wa biashara kwa sasa umewekewa mazingira rafiki hivyo ni wakati muafaka kwa wadau kurasimisha biashara zao kwa njia ya mtandao ili kuwa na mazingira rafiki ya kufanya biashara zao.
"ili kuendelea kiuchumi na kufungua wigo wa biashara urasimishaji wa biashara ni jambo la msingi,"amesisitiza Bw. Girangay.
Amewahimiza wadau kuingia wenyewe kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao( online Registration System-ORS) na wakihitaji usaidizi wawasiliane moja kwa moja na BRELA ili kupata usaidizi badala ya kuwatumia "vishoka" ambao mara nyingi huwapotosha na kusababisha malalamiko.
Aemeeleza kuwa kuna faida nyingi kwa wadau kurasimisha biashara zao kwani biashara inaaminika kwa wateja pamoja na taasisi mbalimbali ikiwemo Serikali yenyewe.

Aidha amezitaja huduma zinazotolewa na BRELA kuwa ni pamoja na usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Makampuni, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma, utoaji wa Leseni za Biashara kundi A na Leseni za Viwanda, utoaji wa Hataza sanjali na uwasilishaji wa taarifa za mwaka kwa kampuni.
Mkutano wa Wakandarasi unaofanyika tarehe 12-13 Mei,2022 jijini hapa umebeba kauli mbiu ya “umuhimu na mchango wa wakandarasi katka uchumi wa Tanzania,”.