Breaking

Friday, 13 May 2022

BREAKING: SIMBA SC YAMTEMA MORRISON




Na Ayoub Julius, Lango La Habari 

Klabu ya Simba Sc imetoa taarifa ya kumpa mapumziko mchezaji raia wa Ghana Benard Morisson hadi mwisho wa msimu taarifa hiyo imetolewa na Simba sc mapema leo tarehe 13 Mei 2022. 


Taarifa ya Simba imeeleza kuwa imefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binafsi.

Aidha Klabu hiyo imetoa shukrani kwa Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumu ndani ya klabu hiyo.

“Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia klabu yetu na kuisadia kupata mafaniko kadhaa ikiwemo kucheza robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, ubingwa wa kombe la shirikisho la Azam Sports, na ubingwa wa kombe la Mapinduzi,” Taarifa ya Simba

Hivi karibuni tetesi mbalimbali zimekuwa zikimuhusisha Benard Morisson kurejea tena kwa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania bara Young African

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages