Na Said Muhibu, Lango La Habari
Mfanyabiashara na mkuu wa Muungano wa Kampuni ya Eldridge Todd Boehl na wenzake wanakaribia kuimiliki klabu ya Chelsea rasmi kufuatia kibali kilichotolewa na serikali ya Uingereza kuipitisha leseni ya mauzo kwa klabu hiyo.
Muungano huo unaoongozwa na Todd Boehly unataka kuashiria mwisho wa enzi ya Roman Abramovich kwa kumpa Tuchel ishara ya wazi kwamba wako makini katika suala la umiliki wa klabu ya Chelsea.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Daily Telegraph limeripoti msemaji mkuu wa serikali ya Uingereza James Slack amesema ameridhia kuuzwa kwa klabu hiyo ijapokuwa mauzo hayo hayatamnufaisha aliyekuwa tajiri na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abrahamovic na badala yake pesa zitatumika kuwasaidia waathirika wa vita kati ya Urusi na Ukraine.
"Kufuatia kazi kubwa, sasa tumeridhika kwamba mapato kamili ya mauzo hayatamnufaisha Roman Abramovich au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa. Sasa tutaanza mchakato wa kuhakikisha mapato ya mauzo yanatumika kwa sababu za kibinadamu nchini Ukraine, kusaidia wahasiriwa wa vita," Alisema.
Mapato kutokana na mauzo ya awali ya pauni bilioni 2.5 yanatarajiwa kuanza kubadilika mara moja huku mawaziri sasa wakitayarisha marekebisho ya leseni ambayo inamaanisha Chelsea inaweza kuuzwa kama mali iliyozuiliwa. Dakika ya mwisho ruhusa ya Uropa, ambayo ilisababisha ucheleweshaji zaidi, ilikuwa muhimu kwa sababu Abramovich pia ameidhinishwa huko na amekuwa na pasipoti ya Ureno.
Aidha Boehly yuko tayari kumpa kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel pauni milioni 200 kutumia msimu huu wa joto mara baada ya kupata umiliki wa asilia 100 wa klabu hiyo.
Kwa upande wake kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel, ameweka wazi kwamba Chelsea italazimika kuchukua hatua za haraka na madhubuti mara tu klabu hiyo itakapoweza kufanya biashara kama kawaida chini ya umiliki wao mpya. Boehly, ambaye alizungumza na Mjerumani huyo na kikosi baada ya ushindi wa siku ya mwisho dhidi ya Watford.