.jpg)
Na lango la habari
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limekamata pikipiki za miguu mitatu maarufu bajaji 84 ambazo madereva wake hawafuati sheria za usalama barabarani.
Akithibitisha hilo Mei 21, 2022 mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Maigwa amesema kuwaa Bajaji hizo zimekamatwa Kupitia Opereshen Maalum za kukamata babaji ambazo madereva wake hawafuati sheria za usalama barabarani
Kamanda Maigwa amesema kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ukiukwaji kwa baadhi ya sheria za usalama barabarani kunakofanywa na madereva wa bajaji kwa kutokufuata na kutii sheria hizo ikiwemo kushusha na kupakia abiria sehemu zisizoruhusiwa, kuzidisha abiria na kushindwa kufuata masharti ya leseni zao za usafirishaji.
Amewataka madereva hao pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo vilivyokamatwa kuleta leseni zao za udereva, kadi za bajaji pamoja na nyaraka za bima ili kuona uhalali wa umiliki wao.
Aidha, ametoa onyo kali huku akiwataka madereva wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kupunguza ajali na kuongeza kuwa operesheni inayofanywa na Jeshi hilo la Polisi ni endelevu.