Breaking

Tuesday, 24 May 2022

AJALI YAUA WATATU NA KUJERUHI 26 MANYARA, DEREVA WA BUS AKIMBIA




Watu watatu wamefariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Mohamed Classic kugongana na uso kwa uso na Fuso Arusha Wilaya ya Hanang' Mkoa wa Manyara.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga amesema ajali huyo imetokea leo Jumanne Mei 24 ambapo fuso lilikuwa limetoka mkoani Tabora kuelekea Kilimanjaro likiwa limebeba mchele ambapo iligongana liligongana uso kwa uso na Basi mohamed Classic katika kijiji cha Ming'enyi wilayani Hanang' mkoani Manyara kwenye barabara ya Singida-Arusha.

Kamanda Kuzaga amesema Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi kutokuzingatia alama za barabarani.


"dereva wa basi ametoroka kusikojulikana tunaendelea kumtafuta kwa kusababisha ajali na kugharimu maisha ya Watu na majeruhi na hatua kali zitachukuliwa" Amesema Kamanda Kuzaga

Aidha ametaja Waliofariki kuwa ni Msaidizi wa dereva wa fuso, Msaidizi wa dereva wa basi pamoja na utingo wake.

"Majeruhi ni Wanaume 14, Wanawake 10 na Watoto wawili ambao wote wapo katika Hospitali ya Tumaini Kateshi"
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages