Breaking

Thursday, 19 May 2022

AHUKUMIWA MIEZI 6 JELA KWA KUWATISHIA WANAWAKE WALIOMKATAA




Mwanariadha wa Ujerumani amehukumiwa kifungo cha Jela miezi sita au kulipa faini ya Ksh. 70,000 (Tsh. Milioni 1.3) kutokana na kosa la vitisho na udhalilishaji wa mtandaoni Nchini Kenya.

Weiss Marvin Valentin, 25, alitenda kosa hilo mwaka 2022 kwa kutoa matamshi ya kukera na kutishia kusambaza picha za kuwadhalilisha za Regina Nguria na Julian Alonso, ambapo aliwataka kimapenzi wakamkataa.

Mashtaka ambayo yalionyesha kusababisha wasiwasi kwa walalamikaji kwamba kitu kibaya kinaweza kuwatokea.


Valentin alishtakiwa kwa makosa manne ya kutuma jumbe za kutatanisha kwa wanariadha hao ambao alitaka wajihusishe nao kimahaba lakini uchumba wake ulikataliwa.

Pia alikabiliwa na shtaka jingine la kueneza taarifa ovu Kinyume na Kifungu cha 112A (1) cha kanuni ya adhabu.

Akiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Iten Caroline Ateya, mwanariadha huyo alikiri makosa hayo manne ambapo alihukumiwa kifungo cha Jela miezi sita au kulipa faini ya Ksh. 70,000 (Tsh. Milioni 1.3) , pia akatakiwa kuondoka nchini humo ndani ya saa 72 baada ya kulipa faini au baada ya kutoka jela ama atashindwa kulipa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages