Mahakama ya Wilaya Nkasi Mkoani Rukwa imemhukumu kifungo cha maisha jela Peter Malema (21) Mkazi wa Kijiji cha Nkundi Kata ya Kipande Wilayani Nkasi kwa kosa la kumbaka Mtoto wa miaka 4.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na Waendesha mashitaka Denis Chagike na Sedrick Mashauri wameieleza Mahakama hiyo kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo March 23, 2021 katika Kijiji cha Nkundi ambapo alimbaka Mtoto huyo wa miaka 4 na kumsababishia maumivu makali.
"Mtuhumiwa hili ni kosa lake la pili la ubakaji na katika kosa la kwanza aliwai kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na aliondolewa baada ya kushinda rufaa"
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya Benedict Nkomola amesema Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani kwa kosa hilo.