Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa leo Aprili 22, 2022 ameshiriki futari maalum jijini Dar es Salaam.
Futari hiyo maalum imeandaliwa na Ubalozi wa Saudi Arabia na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Katika futari hiyo maalum wageni waliohudhuria wameaswa kutenda mattendo mema katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani na baada ya hapo kama ilivyoelekezwa kwenye kitabu kitakatifu cha Qur'an.