Breaking

Saturday, 9 April 2022

WAWILI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NYARAKA




Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kughushi na kutumia mihuri ikiwemo ya uwakili kujipatia kipato isivyo halali.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI amewataja watuhumiwa hwo kuwa ni RAPHAEL STEVEN (34) mfanyabiashara na mkazi wa Uyole Jijini Mbeya na PETER NATHAN (49) mfanyabiashara na mkazi wa Mwakibete Jijini Mbeya.

Kamanda Matei amesema kuwa watuhumiwa walikamatwa Aprili 4, 2022 huko maeneo ya sokoine jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri.

Amesema kuwa, katika upekuzi watuhumiwa walikutwa na mhuri wa uwakili unaomilikiwa na BENARD GWAKISA (35) Wakili wa kujitegemea na mkazi wa Manga Veta.

Aidha ameongeza kuwa Nyaraka nyingine walizokutwa nazo ni nyaraka za mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), BRELA, leseni mbili za biashara kutoka halmashauri ya Jiji la Dodoma, manispaa ya kinondoni na laini za simu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages