Breaking

Monday, 18 April 2022

WASIOJULIKANA WAUA NA KUIBA MAFUTA YA KULA






Polisi katika eneo la Uranga kaunti ya Siaya nchini Kenya, wanachunguza mauaji ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19, baada ya watu wasiojulikana kumvamia dukani na kumuua kisha kuondoka na mafuta ya kula.


Tukio hilo limetokea Jumatano, Aprili 13, 2022, ambapo kwa mujibu wa polisi wameeleza kwamba mwili wa kijana huyo uliokuwa umekatwakatwa vibaya, ulipatikana kando ya barabara, karibu na duka hilo, siku tatu baada ya kuripotiwa kutoweka.

OCPD wa Alego-Usonga Benedict Mwangangi amesema kuwa kijana huyo alikuwa amemaliza mtihani wake wa kidato cha nne (KCSE) 2021, akisubiri matokeo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages