
Na Mwandishi Wetu-Uganda
Mitandao mbalimbali Nchini Uganda imeripoti kuhusu kikundi cha Wanawake jijini Kampala kufanya maandamano wakishinikiza Wanaume zao kuwaongezea kiwango cha pesa ya matumizi wanachowaachia asubuhi (Kodi ya meza maarufu Kameeza) wakidai gharama za maisha zimepanda.
Wanawako wameandamana leo Jumatano April 11, 2022 wakidai kuwa Wanaume hawawapi heshima wanayostahili na hawathamini mchango wao kwenye Familia.
Wamesema licha ya gharama za maisha kuwa juu wanasikitika kuona bado Wanaume wanaendelea kuacha pesa ileile ambayo walikuwa wanaacha zamani
"Kama Mwanaume alikuwa anakuachia Elfu 10 mwaka jana na leo anataka aache ileile bila ya kuwaza kuwa gharama za maisha zipo juu"wamesema
Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini Uganda wamesema Wanawake hao wamekamatwa na kwa sasa wanashikiliwa Kituo cha Polisi Kampala kwakuwa maandamano yao ni batili na hayajazingatia sheria.