Breaking

Sunday, 3 April 2022

SIMBA YATINGA ROBO FAINALI CAF IKIWALIZA USGN 4 - 0


Na Samir Salum - Lango la Habari 

Club ya mpira wa miguu ya SIMBA imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi wa goli 4 - 0 dhidi ya US GENDARMERIE.


Katika mchezo huo uliochezwa leo Jumapili April 03, 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam goli la kwanza la Club ya Simba limefungwa limefungwa Sadio Kanoute dakika ya 63.


Magoli mawili yamepachikwa kambani na Chris Mugalu katika  dakika ya 68 na 78 huku goli la nne likiwa la kujifunga ambapo mlinda mlango wa US Gendarmerie Saidu Hamisu aliuingiza mpira golini kwake baada ya kurudishiwa na beki wa timu yake.


Kutokana na matokeo hayo Club ya Simba inafikisha Alama 10 ambapo katika kundi D inakuwa Nafasi ya pili ikiongozwa na RSB Berkane.


Aidha, nafasi ya tatu inashikiliwa na na ASEC Mimosas Pointi 9 na US Gendarmerie wakimaliza wa mwisho kwa pointi zao 5.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages