Na Ayoub Julius, Lango la habari
Klabu ya Simba sc imeondolewa katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kukubali kichapo cha penati 4-3.
Hatua hiyo inafuatia baada ya Orlando Pirates kupata ushindi wa goli moja lililoofingwa na Peprah mnamo dakika ya 60' na kufanya uwiano wa goli 1-1 ambapo mchezo wa kwanza ulichezwa nchini Tanzania Aprili 17 na Simba Sc kuibuka mshindi kwa goli moja goli ambalo lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Shomari Kapombe mnamo dakika ya 68' ya mchezo.
Simba ndiyo klabu pekee Tanzania iliyofika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika, mwaka 1974 ikiitoa timu ngumu ya Ghana katika Robo Fainali, Hearts Of Oak kwa jumla ya mabao 2-0.
Yalikuwa ni mabao ya Adam Sabu (sasa marehemu) na Abdallah 'King' Kibadeni, mjini Accra, yaliyoipa timu hiyo ushindi wa 2-0, kabla ya kuja kumalizia kwa sare ya bila kufungana nyumbani mjini Dar es Salaam.
Sasa klabu ya Simba Sc inarejea nchini Tanzania kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa dabi dhidi ya Yanga Sc mchezo utaochezwa siku ya Jumamosi Tarehe 30 mwezi Aprili 2022.
Simba inashika nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao wakubwa nchini Yanga Sc wakiwa na alama 41 tofauti ya alama 13 kati yao.