Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini Afrika Kusini Tebogo Motlanthe amesema kitendo cha Klabu ya Simba kutoka Tanzania kuchoma kitu katikati ya Uwanja ni jambo la aibu na si la kiu ana michezo.
Motlanthe amesema kitendo hicho hakikubaliki na tayari kama Shirikisho tayari wameandika barua kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuona hatua stahiki zinachukuliwa.
Klabu ya Simba ilitolewa na Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 katika michezo yote miwili ya hatua hiyo ya mtoano.
Kuhusu suala hilo Ahmed Ally alipoulizwa ni jambo gani ambalo walifanya alijibu kuwa ni siri.
“Ile ni siri ya jando huwezi kusema ilikuwa ni jambo gani bali ni siri ya jando,”