Breaking

Tuesday, 5 April 2022

SERIKALI YAENDELEA KUDHIBITI MIGOGORO YA BINADAMU NA WANYAMAPORI SIMIYU



Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kudhibiti migongano baina ya binadamu na wanyamapori katika maeneo ya kinga ya hifadhi na maeneo ya mtawanyiko wa wanyamapori Mkoani Simiyu.


Hayo yameelezwa leo Jumanne Aprili 5, 2022  na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb)  Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Minza Simon Mjika.


Amesema Wizara hufanya doria za mara kwa mara kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu na pia vituo viwili vya askari vitajengwa katika maeneo ya Busega na Meatu.


Pia, Wizara inatarajia kuajiri askari 600 na mafunzo ya mbinu za kujilinda na kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu yametolewa kwa Halmashauri za wilaya 17.


Aidha, Wizara imetoa namba maalum za simu kwenye kila kanda za kiutendaji ili kuwezesha wananchi kutoa taarifa za matukio ya wanyamapori bila malipo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages