Breaking

Monday, 18 April 2022

RC KAFULILA ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI, AWAPA SIKU 14 KUKAMILISHA



Na Mwandishi Wetu-Simiyu


Mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila, ametoa siku 14 kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri mkoani humo, kuhakikisha wanakamilisha uandikishaji wa anuani za makazi na si vinginevyo.

RC Kafulila amesema hakutakuwa na cha msalia mtume kwa viongozi wa wilaya watakaosalia kujikongoja kukamilisha uandikishaji wa anuani za makazi ya raia, baada ya siku 14 alizotoa kufika ukingoni.

Wakati hayo yakijiri, baadhi ya wananchi na viongozi wa serikali za mitaa wamesema utaratibu huo wa anuani za makazi una faida katika usalama na maendeleo ya wananchi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages