Breaking

Wednesday, 20 April 2022

RALF RANGNICK KUFANYA MAPINDUZI KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED

***********

Na Ayoub Julius-Lango la habari 


Kocha wa muda wa timu ya Manchester United Ralf Rangnick amesema kuwa timu ya Manchester United itafanya mapinduzi makubwa katika kikosi chake katika majira ya joto.


Yote hayo yanajiri baada ya Manchester United kupoteza mchezo wake siku ya Jumanne Aprili 19,2022 dhidi ya mahasimu wao wa muda Mrefu miamba wa Anfield Liverpool kwa bao 4-0. 


Amesema kuwa takribani wachezaji  kumi wanatakiwa kuondoka na kuleta wachezaji wengine wapya watakaoendana na mfumo na falsafa za kocha mpya atakayechukua timu hiyo. 


Kwa siku za hivi karibuni Kocha wa Ajax raia wa Uholanzi Erik Teg Hag amehusishwa kwa karibu sana kuchukua mikoba ya Rangnick na mpaka sasa hatua za mwisho za kukamilisha mkataba wake zikiwa zinafanyika. 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages