Breaking

Saturday, 2 April 2022

RAIS SAMIA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUTOKUWA NA HESHIMA YA UOGA.."SIJAUMBWA KUFOKAFOKA"





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi na watumishi wa umma kuwa na heshima ya kweli kutoka ndani ya mioyo yao na kila mtu kutimiza majukumu yake kwa maadili na weledi mkubwa kwa maslahi mapana ya taifa letu.


Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi April 02, 2022 jijini Dodoma wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali walioteuliwa hivi karibuni ikiwa pamoja na mawaziri waliobadilishwa kutoka wizara moja kwenda nyingine.

Katika hotuba yake Rais Samia ameabainisha kuwa licha ya serikali ya awamu ya tano kusifiwa kwa kukuza heshima kwa watumishi wa umma, lakini heshima hiyo ilikuwa ya woga, na hivyo akawataka watumishi kuwa na nidhamu kutoka ndani ya mioyo yao.

“Tunasifiwa kuwa awamu ya tano tulikuza heshima kwa watumishi wa umma, heshima iliyokuzwa ni heshima ya woga kwa sababu alikuwepo simba wa Yuda, ambaye ukimgusa sharubu anakuraruwa, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni” amesema Rais Samia Suluhu Hassan

Aidha Rais Samia amesisitiza kuwa ataendelea kufanya kazi kwa kalamu, na kamwe hawezi kuwafokea watendaji walio chini.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages