Katika kuadhimisha Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Rais Samia Suluhu Hassan amewasamehe wafungwa wapatao 3,826 kwa masharti mbalimbali.
Msamaha huo utahusisha Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya usafirishaji wa Dawa za Kulevya ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka 20 na kuendelea
Aidha, pia utahusisha Wafungwa wanaotumikia adhabu kwa makosa ya wizi au ubadhirifu wa Fedha na Mali za Umma ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka 15 na kuendelea