
Rais Samia ameeleza hayo leo Jumanne Aprili 5, 2022 Jijini Dodoma wakati akizindua mkutano huo wenye lengo la kujadilili maeneo matatu ya mardhiano, haki na amani.
Mkutano huo wa siku mbili utahusisha kumkabidhi uenyekiti wa TCD, Abdulrhaman Kinana baada ya Zitto Kabwe kumaliza muda wake.
Akitoa ombi la marekebisho hayo Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia (TCD) anayemaliza muda wake, Zitto Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, amesema kuwa Julai mwaka huu Tanzania inatimiza miaka 30 tangu kurejea katika demokrasia ya mfumo wa vyama vingi hivyo ingependeza wakati wa mmadhimisho kuwepo na marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa.
“Kama itakupendeza Mheshimiwa Rais na kama taratibu za Serikali zitakuwa zimekamilika kufuatia taarifa ya Kikosi Kazi, tutafurahi tutakapokuwa tunaadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi tuwe tumefanya maboresho ya sheria ya vyama vya siasa,” amesema Zitto.

“Itategemea mtakavyotuletea na Serikali itakavyochuja kwenye mazingira yetu, kama hayatakuwa na shida, lakini yakiwa na shida itabidi tukutane kikao na kikao… hadi tufike. Kama hayatakuwa na shida tutamaliza kwa muda huo Ili tuseme sheria yetu tumeibadilisha baada ya miaka 30, hii halina shida,” amesema Rais Samia

Rais Samia ameongeza kuwa Tanzania haitajengwa na mtu mmoja au chama kimoja bali itajengwa na Watanzania wote.
Amesema Nchi ilichagua kuingia mfumo vyama vingi ili kuwezesha kupatikana maendeleo kwa haraka kulingana na maono ya wingi wa vyama hivyo ambavyo vitatoa maoni pindi vitakapoona mapungufu na kuisaidia Serikali kuyatatua.
"kwenye mfumo wa vyama vingi, macho yako mengi, maono yapo mengi wanavyoona chama kimoja ambacho kipo ndani ya serikali pengine hawatokuwa na macho makubwa ya kuona kama wengine walio nje ya Serikali, na ndio maana tukasema vyama vingi hivi kazi yake ni kuangalia yanayoendelea ndani ya Serikali na kutoa maoni yao"
"kwenye mfumo wa vyama vingi, macho yako mengi, maono yapo mengi wanavyoona chama kimoja ambacho kipo ndani ya serikali pengine hawatokuwa na macho makubwa ya kuona kama wengine walio nje ya Serikali, na ndio maana tukasema vyama vingi hivi kazi yake ni kuangalia yanayoendelea ndani ya Serikali na kutoa maoni yao"
"Tanzania haitajengwa na mtu mmoja na chama kimoja. Wote kama Watanzania lazima tujadili mambo yetu iwe sera, sheria, dira lazima tujadili wote kama Watanzania" amesisitiza Rais Samia
Aidha amewataka wajumbe wa mkutano huo kuweka mbele utaifa na kuzingatia mazingira yaliyopo hapa nchini na kutoa angalizo kuwa hakuna atakayewasaidia katika mchakato huo isipokuwa Watanzania pekee.
“Tunapozungumza maridhiano, tunayazungumza vipi au tunaridhiana wapi? Katika maeneo yapi na tunakwenda hadi wapi? Au Haki zetu ni zipi Watanzania haki zetu ni zipi kama vyama vya siasa. Tutazungumza haki zetu na pale ilipobinywa tuzungumze namna ya kuifungua lakini kwa mazingira ya Utanzania" amesisitiza Rais Samia