Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznnia Samia Suluhu Hassan ameagiza ameiagiza Wizara ya Kilimo kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango, kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumatatu April 04, 2022 wakati akizindua uhawaji wa vitendea kazi vya maafisa ugani kilimo ikiwemo pikipiki, vifaa vya kupima afya ya udongo, simu janja na visanduku vya ufundi kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Dodoma.

Rais Samia amesema Mfuko huo utachangiwa na tozo maalum kwenye mazao ya kilimo, Mfuko Mkuu wa Sefikali na wadau wa maendeleo.
Amesema mfuko huo utakuwaa na majukumu ya kugharamia pembejeo za kilimo kama ilivyofanyika kwenye korosho, pamba na tumbaku ili mfuko huo utumike kama ruzuku pindi pembejeo zinapopanda bei.

Pia Ameiagiza Wizara hiyo na Ofisi ya Rais Utumishi kupitia upya na kuufanyia mabadiliko muundo wa Tume ya Umwagiliaji ili kuhakikisha inakuwa na Ofisi katika kila Wilaya.
Kwa upande mwingine, Rais Samia ameagiza mashamba yote ambayo yapo Chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kufufuliwa na kuaza kutumika kwa kushirikiana na Sekta binafsi kupitia mfumo wa kukodisha ardhi kwa muda mrefu.

Aidha, Rais Samia ameitaka Wizara ya kilimo kuweka msukumo kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na kuwa ya kibiashara, ikiwemo mazao ya mboga mboga pamoja na mazao ya kimkakati ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza ziada nje ya nchi.
Rais Samia amesema Sekta va kilimo nchini imeendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa ambapo kwa mwaka 2020 sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 4.9 kuchangia kwa asilimia 26.9 katika pato la taifa, kuchangia kwa asilimia 61.1 katika kutoa Ajira kwa Watanzania na kuchangia kwa asilimia 65 ya malighafi za viwandani.