Breaking

Monday, 4 April 2022

MBAPPE AFUNGUKA JUU YA HATIMA YAKE KWENYE SOKA

 


Na Ayoub Julius - Lango la Habari  


Mshambuliaji machachali wa PSG na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe amefunguka juu ya hatma yake katika maisha yake ya kusakata kabumbu. 


Akizungumza katika mtandao maarufu wa kimarekani Prime Video Kylian Mbape amefunguka kuhusu hatima yake kati ya Real Madrid na Paris Saint-Germain. 


Amesema kuwa bado hajafanya maamuzi yake kuhusu maisha yake ya soka ya baadae kwani bado anajadiliana na Familia yake na kuwa kuna mambo mengi ya kutafakari na kama angelifanya maamuzi angelikuwa tayari ameshatangaza kwa mashabiki wake. 


Aidha ameongeza kuwa hataki kufanya makosa kwani bado anajaribu kufanya maamuzi yaliyosahihi kwa maisha yake ya baadae. 


Kwa siku za hivi karibuni Miamba wa Hispania Real Madrid wameonyesha nia ya kuitaka huduma ya kinda huyo wa kimataifa wa ufaransa ambae hajasaini mkataba mpya na PSG ambapo mkataba wake wa awali utafikia tamati tarehe 30 mwezi Juni.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages