Breaking

Friday, 29 April 2022

MATUNDA YA ROYAL TOUR: MTAYARISHAJI HOLLYWOOD KUWANOA WADAU WA FILAMU DAR

Ni kama vile matunda ya Filamu ya Royal Tour yanazidi kuanza kuonekana kwa sekta mbalimbali ambapo leo sekta ya sanaa inaanza kunufaika.


Mtayarishaji maarufu kutoka California Marekani, John Feist ambaye pia ni Mshindi wa tuzo ya Emy (Emy Award), leo Ijumaa April 29, 2022 jijini Dar es Salaam anatoa semina kuhusu masuala mbalimbali ya kuboresha kazi za filamu hapa nchini.


Kwa wasiomjua Feist ameshiriki kutayarishaji filamu mbalimbali ikiwemo Survivor na makala mbalimbali za filamu katika National Geographic.


Aidha, Bw. Feist ndiye mtayarishaji na mwandishi wa miswada ya filamu zote za Royal tour zilizopata kuandaliwa sehemu mbalimbali duniani katika kipindi cha miaka 22 iliyopita na kutoka katika nchi mbalimbali zaidi ya 8 ikiwemo Tanzania ambayo sasa ni ya 9.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages